• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Azevêdo kuondoka kwenye wadhifa wake mapema kwa mwaka mmoja

    (GMT+08:00) 2020-05-15 10:13:20

    Kwenye mkutano maalumu wa Shirika la biashara duniani (WTO) uliofanyika jana kwa njia ya video, ambao umeshirikisha wajumbe 164 kutoka nchi wanachama, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Roberto Azevêdo ametangaza kuwa ataondoka madarakani rasmi tarehe 31 mwezi Agosti mwaka huu, na kumaliza muda wake mapema kwa mwaka mmoja kuliko ilivyopangwa.

    Bw. Azevêdo amesema huu ni uamuzi binafsi na wa familia yake, ameeleza imani yake kuwa uamuzi huo unaendana na maslahi mapana ya WTO.

    Vilevile amewapendekeza wanachama wa WTO wachague mapema mkurugenzi mpya, ili kufanya maandalizi kwa mkutano wa 12 wa mawaziri wa WTO utakaoahirishwa hadi mwaka kesho kutokana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako