• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Eymael aukwepa mtego wa Zahera Yanga SC

  (GMT+08:00) 2020-05-15 16:57:53

  Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, ameweka wazi kwamba katika kikosi chake cha msimu ujao atakachofanya ni kutosajili wachezaji wengi badala yake atafanya maboresho tu kidogo. Eymael amesema hahitaji wachezaji wengi katika kikosi chake cha msimu ujao badala yake analenga kuchukua wachezaji wachache ambao watakuja kuongeza nguvu kwa waliopo sasa. Eymael ameongeza kwamba hatafanya kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo kikosi hicho kilisajili zaidi ya wachezaji 11 kwenye dirisha kubwa la usajili wakati kocha mkuu akiwa Mwinyi Zahera raia wa DR Congo. Amesema mipango yake kwa sasa ni kuongeza nguvu mpya za wachezaji wachache katika wale ambao wamebakia kwa ajili ya kuifanya timu hiyo kwa msimu ujao kuwa na nguvu ya kupambana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako