• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Man United yamtengea Dembele pound milioni 60

  (GMT+08:00) 2020-05-15 16:58:14

  Klabu ya Manchester United, ina uhakika wa kutoa kiasi cha pauni 60m kwa ajili ya kumsajili straika Moussa Dembele wa Klabu ya Lyon ya Ufaransa. United imekuwa ikimfuatilia staa huyo zaidi ya miezi 12 sasa na ilituma wafuatiliaji wake kuangalia uwezo wake na sasa wameridhika. Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solsjkaer anaamini kabisa kuwa staa huyo ndiyo atakuwa mbadala sahihi wa nafasi ya Romelu Lukaku ambaye alitimka kwenye kikosi hicho na kwenda Inter Milan. Hata hivyo, timu ya Lyon ambako Dembele anakipiga msimu ujao haitashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kumaliza nafasi ya saba huku ligi yao ikifutwa kutokana na janga la Virusi vya Corona. Rais wa Klabu ya Lyon, Jean Michel Aulas alikiri kuwa hawezi kuzuia mchezaji aondoke ndani ya kikosi chake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako