• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Newcastle United kutoa fedha nyingi kumsajili Gareth Bale

  (GMT+08:00) 2020-05-15 16:58:35

  Newcastle United wapo tayari kuweka mezani kiasi cha Sh8 bilioni ili kujinasia huduma za fowadi matata wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale mwishoni mwa msimu huu. Kufaulu kwa mipango yao hiyo kutamshuhudia Bale ambaye uhusiano wake na kocha Zinedine Zidane umevurugika uwanjani Santiago Bernabeu akirejea katika Ligi Kuu ya Uingereza, miaka saba tangu aagane na Tottenham Hotspur. Kwa mujibu wa gazeti la FourFourTwo nchini Uingereza, kati ya vikosi vitatu ambavyo kwa sasa vinafukuzia saini ya Bale, ni Newcastle ndio ambao wameelekea kushangaza zaidi mashabiki. Mbali na Newcastle, klabu nyinginezo zinazomhemea Bale ni Inter Miami ya kocha David Beckham na Spurs ambao wako radhi kumrejesha nyota huyo jijini London kwa kiasi cha Sh7 bilioni kwa matarajio kwamba atastaafu ulingoni akivalia jezi zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako