• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kipa KMC atamani Ligi Kuu

  (GMT+08:00) 2020-05-15 16:59:07

  Mlinda mlango wa timu ya KMC inayoshiriki ligi Kuu Tanzania Bara, Denis Richard, amesema upweke wa kufanya mazoezi ya kipekee unamfanya atamani ligi irejee ili aweze kujumuika pamoja na wenzake. Denis kabla ya kutua KMC kwa watoto wa Kinondoni aliwahi kukipiga kwa vinara wa Ligi hiyo Simba na kujikuta akikosa nafasi ya kuonyesha uwezo wake na kulazimika kuangalia maisha mapya. Denis amesema, kwa sasa yeye anajifua katika fukwe za Escape Jijini Dar es Salaam ili kulinda kiwango chake wakati huu ligi imesimama. Amewasisitizia wachezaji wenzake huko majumbani waliko wasibweteke bali watumie muda huo wa kukaa nyumbani kujilinda viwango vyao. KMC ina makipa watatu Juma Kaseja, Jonathan Nahimana na Denis.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako