• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mshambuliaji Harry Kane adhamini jezi za kikosi cha Leyton Orient msimu ujao

    (GMT+08:00) 2020-05-15 16:59:52

    Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane, amedhamini jezi za kikosi chake cha zamani cha Leyton Orient kwa minajili ya kampeni za msimu ujao. Kane, 26, aliwajibishwa katika kikosi cha watu wazima kambini mwa Orient kwa mara ya kwanza mnamo 2011. Kwenye mikono ya jezi hizo, maandishi ya kuwapongeza maafisa wa afya wa hospitali ya Mind and Haven House Children's Hospice, Uingereza yataandikwa katika hatua ya kutambua juhudi zao katika kupambana na janga la corona. Nembo ya hospitali hiyo itatiwa pia kwenye sehemu ya kifua ya jezi, karibu na ilipo nembo ya klabu ya Orient. Kane alikuwa na umri wa miaka 17 pekee alipoingia katika sajili rasmi ya Orient kwa mkopo kutoka Tottenham. Katika kipindi hicho cha mkopo, alipachika wavuni jumla ya mabao matano kutokana na mechi 18 kabla ya kurejea Tottenham ambapo nyota yake ilianza kung'aa zaidi kitaaluma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako