• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Roke Telkom ya Uganda yachangia hazina ya kupambana na Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-15 20:19:23

    Kampuni ua mawasiliano ya Roke Telkom nchini Uganda imetoa mchango wake wa shilingi milioni 20 za Uganda kwa hazina ya taifa ya kupambana na virusi vya Corona. Akitoa fedha hizo kwa waziri katika ofisi za waziri mkuu Bi Mary Okurut, afisa mkuu wa kampuni hiyo Bw Michael Mukasa amesema Roke Telkom Roke ni mali ya Waganda na hivi sasa wanasimama pamoja na serikali kuhakikisha kuwa kwa pamoja wanakabiliana na virusi vya Corona ili kuwaokoa waganda.Pia Roke imeipongeza serikali ya Uganda kutokana na juhudi zake za kukabilian ana maambukizo ya virusi vya Corona.Serikali ya Uganda katika siku za hivi karibuni imekuwa ikipokea misaada ya chakula vifaa vya matibabu pamoja na fedha kutoka kwa wahisani nchini humo. Roke Telkom imekuwa ikiendelea kuwasaidia waganda kupata inteneti kwa gharama nafuu wakati huu ambapo nchi inapambana na janga la Corona.Aidha Roke imewataka Waganda kufuata maagizo ya serikali katika vita dhidi ya Corona nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako