• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya mafuta yapunguzwa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2020-05-15 20:28:58

    Wamiliki wa magari nchini Kenya wamefurahia hatua ya kupunguzwa kwa bei ya mafuta kwa shilingvi 20 kwa lita moja ya kila aina ya mafuta. Taarifa hiyo ya kupunguzwa kwa bei ya mafuta inakuja wakati ambapo bei ya mafuta ghafi inaonekana kushuka katika soko la kimataifa kwa zaidi ya miaka miwili. Mamlaka ya kudhibiti bei ya mafuta nchini Kenya EPRA imepunguza bei ya mafuta ya Dizeli kwa shilingi 19.9 kwa lita moja ya mafuta hayo hatua ambayo imewafanya wasafirishaji na watengenezaji bidhaa kupata afueni. Mafuta ya petrol yamepunguzwa kwa shilingi 9.54 huku yale ya taa yakipunguzaw kwa shilingi 2.49 kwa lita moja. Kutokana na mabadiliko hayo ya bei sasa bei ya mafuta ya petrol aina ya Super yatakuwa yakiuzwa kwa shilingi 83-33 wakati yale ya dizeli yakiuzwa kwa shilingi 78.37.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako