• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Bayern Munich waanza kwa kuibamiza Union Berlin 2-0 ugani Ander Alten Forsterei

  (GMT+08:00) 2020-05-18 08:19:41

  Viongozi wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) Bayern Munich wamerejea katika mtanange huo kwa mbwembwe zote baada ya kuwacharaza Union Berlin 2-0 ugani Ander Alten Forsterei. Robert Lewandowski aliwafungulia Bayern ukurasa wa mabao kupitia penalti katika dakika ya 40 kabla ya Benjamin Pavard kukizamisha kabisa chombo cha wenyeji wao mwishoni mwa kipindi cha pili. Michuano hiyo imeruhusiwa kurejea bila mashabiki, na watu wengi waliokuwepo nje ya uwanja wamevaa barakoa na hakukuwepo shangwe la kusherehekea ushindi. Bao la Lewandowski lilikuwa ni la 40 katika mechi 34 alizochezea Bayern katika msimu huu. Goli la Pavard lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Joshua Kimmich. Kuahirishwa kwa kampeni za Bundesliga kulifanyika wakati Bayern ambao bado wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 58, huku wakijivunia fomu nzuri iliyowawezesha kusajili ushindi mara 10 kwa kucheza jumla ya mechi 11 mfululizo. Kabla ya kuvaana na Union Berlin, mchuano wao wa mwisho kutandazwa katika Bundesliga ulikuwa dhidi ya Augsburg waliopokea kichapo cha 2-0 ugani Allianz Arena mnamo Machi 8.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako