• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: FC Seoul yaomba radhi kwa kutumia midoli kama Samantha kushabikia mechi

  (GMT+08:00) 2020-05-18 08:20:11

  Klabu ya FC Seoul nchini Korea Kusini imeomba msamaha kwa kutumia midoli kama 'Samantha' kujaza viti ambavyo kwa kawaida, hukaliwa na mashabiki wanaofika uwanjani kuhudhuria mechi. Kwa mujibu wa mtandao wa rt.com, FC Seoul ilijaza midoli kwenye viti vya uwanja wao wa nyumbani mnamo Mei 17, 2020, kabla ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Gwangju FC. Ilihitaji macho makali ya mashabiki kutambua kwamba midoli hiyo ilikuwa ya mapenzi na punde wakajibwaga kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kutaka kujua kiini cha hatua hiyo ya FC Seoul ambayo awali usimamizi ulisisitiza kwamba walikuwa wakitangaza mavazi mbalimbali ambayo midoli hiyo ilivalishwa. Cha kushangaza ni jinsi mashabiki walivyobaini kwamba midoli hiyo hutumiwa katika masuala ya ngono. Hata hivyo vinara wa FC Seoul wamekiri makosa na kutumia mtandao wa Instagram kuomba radhi huku wakishikilia kwamba mkandarasi aliyetakiwa kuupamba uwanja wao kwa midoli ya kawaida, alichanganyikiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako