• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Dortmund yaitandika Schalke Bundesliga ikirudi

  (GMT+08:00) 2020-05-18 15:54:28

  Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, iliyosimama kwa takribani siku 65 kutokana na janga la virusi vya corona, ilirudi kwa kishindo jana huku mabao 12 yakifungwa ikiwemo ushindi wa mabao 4-0 ambao Borussia Dortmund walipata dhidi ya Schalke 04. Ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili msimu huu baada ya ule wa kwanza kumalizika kwa timu hizo kutofungana, mtanange huo ulimalizika kwa Dortumund kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0. Aidha, kiboko ya vigogo Bundesliga, RB Leipzig walipepetana na Freiburg lakini walilazimika kusubiri hadi dakika ya 77 kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji raia wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen, hivyo timu hizo kugawana pointi kwa sare ya 1-1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako