• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: ZAA ipo tayari kimataifa

  (GMT+08:00) 2020-05-18 15:54:45

  Uongozi wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAA), umesema upo tayari kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa. Kaimu Katibu Mkuu wa ZAA, Yassin Muhidini alisemaushiriki wao ni katika riadha ya mbio fupi. Alisema kuwa, mpango wa ZAA ni kuhakikisha inapata nafasi ya kushiriki mashindano ya kusaka viwango vya kufuzu michezo ya Olimpiki ijayo. Amesema lengo lao ni kuhakikisha kila mashindano ya kusaka viwango yatakavyotakangazwa katika nchi mbalimbali, watakuwa wanapeleka wanariadha wao ili washiriki kikamilifu na kupata nafasi ya kushiriki michezo ya Olimpiki. Alisema ili kufikia malengo hayo, wanariadha wenyewe wanatakiwa kujituma kwa bidii kufanya mazoezi yao binafsi kwa kufuata program za mazoezi wanazopewa na makocha wao .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako