• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KICKBOXING: Mashindano ya kickboxing ya vijana kuanza nchini Tanzania

  (GMT+08:00) 2020-05-18 15:56:06

  Mcheza Kickboxing maarufu nchini Tanzania, Japhat Kaseba amesema kuwa, ana mpango wa kuandaa mashindano ya vijana ya mchezo huo, ambayo yatafanyika baada ya tamko la Serikali la kuruhusu mikusanyiko ya watu, ikiwamo michezo. Machi 17 mwaka huu, Serikali ilipiga marufuku mikusanyiko ya watu, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vya corona. Kaseba alisema lengo ni kuchagua timu ya vijana ambayo itaandaliwa kwa ajili ya kushiriki mashidano ya kimataifa. Kaseba alisema kuwa, mpango uliopo ni kuendelea kuhamasisha vijana wengi waweze kujitokeza kujifunza mchezo huo, kutoka katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Alisema kuwa, matarajio yao kuona Tanzania inakuwa na nyota wengi ambao wataitangaza vyema Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako