• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Yanga yaahidi kutikisa

  (GMT+08:00) 2020-05-18 15:55:44

  Klabu ya Yanga nchini Tanzania, imewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea burudani zaidi katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara. Ligi Kuu ambayo imesimama tangu Machi 17, mwaka huu, baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyiko ya watu ikiwemo michezo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka maambukizi ya vizuri vya corona. Hadi ligi hiyo inasimama, baadhi ya timu zimecheza mechi 28, nyingine 29, huku Yanga pekee ikiwa imecheza michezo 27 na kukamata nafasi ya tatu, baada ya kukusanya pointi 51. Ofisa Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, aliwataja mashabiki wao 'kukaa mkao wa kula', kwani kikosi chao kitarejea na makali zaidi. Alisema kuwa, kutokana na mazoezi wanayofanya wachezaji wao, anamini watacheza mpira wa burudani na ufundi sambamba na kushinda michezo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako