• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wafanyibiashara Mtito Andei waumia.

    (GMT+08:00) 2020-05-18 19:26:15
    Wafanyibiashara katika eneo la Mtito Andei katika barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi wanasema wanaendelea kukadiria hasara kubwa kufuatia kufungwa kwa kaunti za Mombasa, Kwale, na Kilifi.

    Aidha zaidi ya wafanyabiashara 500 wanaofanya biashara mbalimbali ikiwemo kwenye mikahawa, vituo vya mabasi, wauzaji wa asali na bidhaa zingine walisema wanaendelea kukadiria hasara baa da ya janga la Covid-19 kufanya shughuli nyingi kukwama.

    Serikali ilifunga kaunti ya Mombasa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Kaunti ya Mombasa ndiyo kitovu cha biashara mbalimbali za Pwani ikiwemo bandari, utalii na uchukuzi.

    Lakini tangu kaunti hiyo ifungwe, hakuna biashara zinazoendelea katika kaunti zinazotegemea Mombasa kwa biashara, hususan sekta ya uchukuzi.

    Mtito Andei huwa ni eneo lililo karibu na mbuga ya wanyama ya Tsavo Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako