• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Watanzania wasihofu. Kuna sukari.

  (GMT+08:00) 2020-05-18 19:26:34
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, amewahakikishia Watanzania kwamba hakutakuwa na uhaba wa sukari tena, na kuwataka wananchi wasiwe na hofu kwani bidhaa hiyo ipo nchini. Aidha, waziri amewaomba wauzaji kutumia bei elekezi ya bidhaa hiyo iliyotolewa na serikali.

  Bashungwa alizungumza wakati akishuhudia shehena ya sukari tani 20,000 iliyowasili katika Bandari ya Mwanza nchini Tanzania, kutoka Uganda mwishoni mwa wiki jana.

  Ameongeza kuwa licha ya sukari hiyo kushushwa Mwanza, pia na mkoa wa Dar es Salaam wanaedelea kushusha. Tayari mikakati imewekwa kuhakikisha kwamba hakutakuwa na kupanda kwa bei ya sukari kote nchini. Mfanyibiashara yeyote atakayepatikana na hatia ya kupandisha bei ya sukari, atachukuliwa hatau kali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako