• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EAC: Mataifa ya EAC yakopa takriban dola bilioni 2.3 kukabili corona.

  (GMT+08:00) 2020-05-18 19:26:55
  Imebainika kwamba mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki yamechukuwa mkopo wa takriban dola bilioni 2.3 ili kukabili janga la virusi vya corona.Hii ni licha ya kuwa mataifa haya yanakumbwa na wakati mgumu kukusanya ushuru baada ya sekta ya biashara kuyumbishwa na virusi vya corona.

  Mkopo wa juu zaidi ulichukuliwa kutoka kwa Shirika la Fedha Duniani. Taifa la Kenya limechukuwa mkopo watakriban dola bilioni 1.5, likiwa ndilo aifa lenye mkopo wa juu zaidi kati ya mataifa sita ya ukanda huu, tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha virusi vya corona tarehe 13 mwezi Machi mwaka huu.

  Uganda imeongeza dola milioni 540.2 kwenye deni lake kwa shirika hilo, huku Rwanda ikiwa na mkopo wa dola milioni 223.6.

  Rais wa Tanzania, John Magufuli, ametoa wito wa kufutiliwa mbali kwa madeni yote ya Tanzania, kutoka nje. Burundi na Sudan Kusini bado hawajatangaza mikopo yao mipya kipindi hiki.

  Kabla ya janga la virusi vya corona, mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki yalikuwa na mkopo kwa Shirika la Fedha Dunia, kima cha dola bilioni 110 kwa pamoja. Kwa miezi mitatu iliyopita, tangu mlipuko wa virusi vya corona, ukanda wa Afrika mashariki kwa jumla una mkopo wa dola bilioni 2.26 kwa Shirika la Fedha Duniani.

  Ikumbukwe kwamba makubaliano ya mataifa ya Ukanda wa Afrika mashariki ni kwamba, hakuna taifa linapswa kuchukuwa mkopo zaidi ya asilimia 50 ya mapato yake ya kitaifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako