• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EAC: Kupunguzwa kwa bei ya mafuta kutawafaa wanaafrika mashariki.

  (GMT+08:00) 2020-05-18 19:27:23
  Mataifa ya Afrika Mashariki yana nafasi nzuri ya kufaidika kutokana na kupunguzwa kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

  Kupungua huku kutaisaidia kuzuia makali ya mfumuko wa bei za bidhaa nyingi, haswa wakati huu wa janga la virusi vya corona. Wanaotarajiwa kunufaika zaidi ni wazalishaji wa bidhaa mbali mbali viwandani ambao hutumia mafuta haya.

  Changamoto kuu na mataifa ya Afrika Mashariki ni ukosefu wa hifadhi ya mafuta mengi, haswa wakati kama huu bei ya soko la kimataiofa ikiwa chini mno. Wasomi wa uchumi wanasema kwamba, hii ni fursa ya kipekee ambayo mataifa ya Afrika mashariki wangeitumia vizuri ila hawana uwezo wa kuhifadhi mafuta mengi.

  Kwa mfano, kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, bei ya mafuta nchini Kenya haijawahi kuwa ya chini kama ilivyo kwa sasa. Lita moja ya dizeli ilipunguzwa kwa dola 0.17 ambayo ni sawa na shilingi 19.19, za Kenya. Kwa sasa, dizeli lita moha nchini Kenya inauzwa dola 0.72, sawa na shilingi 78.37 za kenya.

  Kupunguzwa kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa ina maana kwamba, mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki yataagiza bidhaa za petroli kutoka nje kwa bei ya chini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako