• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Bondia Fabian Lyimo aeleza sababu za kuzuiwa kupigana Marekani

  (GMT+08:00) 2020-05-19 08:46:04

  Bondia Fabian Lyimo ameeleza chanzo cha kupigwa marufuku kuzichapa nchini Marekani. Lyimo amezuiwa na bodi ya kusimamia ngumi nchini humo ambayo imeeleza kumsimamisha kucheza kwenye mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia. Akizungumzia suala hilo kutoka Marekani anakoishi, Lyimo amesema zuio hilo limetokana na kipigo cha KO alichokipata hivi karibuni. Amefafanua kuwa utaratibu ulivyo ni kama bondia amepigwa sana wanamuwekea pingamizi ili asiweze kupigana nchi yoyote utakayokwenda kwani rekodi zitaonyesha umesimamishwa, na ndicho kilichomtokea na yeye. Amesema tayari ameanza mchakato wa kufuta pingamizi hiyo kwa mujibu wa sheria za ngumi nchini humo ambako kwa sasa ndiko anakoombea kibali cha kucheza mapambano ya ndani na nje ya nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako