• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hudson-Odoi anasa kwenye mtego hatari wa corona baada ya kumwalika mrembo

    (GMT+08:00) 2020-05-19 08:46:50

    Callum Hudson-Odoi anatarajiwa kukosa mazoezi ya kwanza ya vikundi vidogo vya wachezaji yatakayoanza Mei 19 baada ya kuvunja sheria za kutotangamana na watu wakati huu wa janga la virusi hatari vya corona. Winga huyu mwenye umri wa miaka 19, ambaye alipatikana na virusi hivyo mwezi Machi kabla ya kupona mapema Aprili, alikamatwa Mei 17 asubuhi baada ya kualika mwanamke nyumbani kwake. Mwanamke huyo, ambaye anasemekana alifika kwa Hudson-Odoi jioni, aliwahishwa hospitali kwa sababu alikuwa akijihisi vibaya. Gazeti la The Sun lilidai kuwa mwanamke aliyekuwa na Hudson-Odoi ni mwanamtindo, ambaye walikutana naye mtandaoni na kisha kualikwa. Hudson-Odoi huenda akaadhiwa vikali na klabu yake kwa kuifanya ionekane vibaya, hasa baada ya klabu hiyo kuonyesha kujituma zaidi katika vita dhidi ya maambukizi ya corona. Mchezaji huyu mwenye asili ya Ghana hulipwa mshahara wa Sh23.4 milioni kila wiki uwanjani Stamford Bridge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako