• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: ZFF yasema imepewa dola 3500 kati ya dola milioni moja

    (GMT+08:00) 2020-05-19 18:10:22

    Msemaji wa Shirikisho la Soka la Zanzibar ZFF, Adam Natepe amesema kuwa wamefanya juhudi kubwa kuongea na Shirikisho la Soka Tanzania TFF juu ya haki zao za fedha za FIFA lakini wenzao wanaonesha kiburi. Natepe amesema kuwa haki ya fedha zao iko katika katiba ya mashirikisho yote mawili hivyo, TFF warejee katika katiba na kusoma makubaliano yao ili wapewe stahiki kwa mujibu wa kanuni. Amesema yapo mambo baadhi serikali ya Tanzania na serikali ya Zanzibar yanakaa pamoja kuyashughulikia na yanakwenda vizuri, lakini katika suala hilo inakuwa sivyo. Amesema katika mipango ya FIFA Forward 1 na FIFA Forward 2, kiasi ambacho ZFF imepewa si zaidi ya dola za Kimarekani 3500 kati ya Dola milioni moja zinazokuja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako