• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Biashara ndogo na ndogo nchini Uganda zinakabiliwa na hali mbaya, kufikia sasa kulingana na ripoti ya EPRC tayari biashara nyingi zimeshuka kwa asilimia 50

  (GMT+08:00) 2020-05-19 19:43:58
  Biashara ndogo na ndogo nchini Uganda zinakabiliwa na hali mbaya baadaye ya ripoti mpya kuonya kuwa hatua za kufungwa kwa sasa kwa nchi ikiendelea kwa miezi sita ijayo basi uenda watu wengi wakafunga biashara zao.

  Ripoti kutoka kwa Kituo cha Utafiti wa sera ya Uchumi (EPRC) iliyoko katika Chuo Kikuu cha Makerere inaonyesha kwamba biashara nyingi tayari zimeshuka kwa asilimia 50.

  Hii inahusishwa na hatua kama vile vizuizi vya usafiri, kukaa nyumbani, kukaa umbali wa mita 1.5 na mwezio na kupigwa marufuku kwa soko la kila wiki, ambayo imezuia wakulima kufanya biashara zao katika masoko.

  Matokeo ya ripoti yanaonyesha kuwa wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini ndio wameathirika zaidi na janga hili la virusi vya corona ikilinganishwa na biashara kubwa.

  Ripoti inasema endapo janga hili la corona litaendlea kwa miezi sita ijayo basi uenda wafanyikazi wapatao milioni 3.8 wakapoteza kazi zao kwa muda na 600,000 kupoteza kazi zao kabisa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako