• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Benki zakabiliwa na Faini ya sh milioni 2 za kuwanyima wakopaji waliooredheshwa vibaya na CRBs

  (GMT+08:00) 2020-05-19 19:44:36
  Benki, saccos na wakopeshaji wadogo wa kifedha sasa wanakabiliwa na faini ya Sh2 milioni kwa kila aliye kosa kulipa deni na amenyimwa mkopo kwa kuorodheshwa vibaya na ofisi ya kumbukumbu ya mkopo ya nchi (CRBs).

  Sheria hii mpya inawakilisha jaribio mpya la kufungua mkopo kwa mashirika na wafanyikazi walio na wakati ngumu kutokana na athari za janga la corona.

  Hazina imeanzisha faini hiyo katika kanuni zinazolenga kusafisha orodha mbaya ya CRB na kuongeza nafasi za wakopaji kuweza kukopa zaidi.

  Benki na saccos wamekuwa wakisita kutoa mikopo kwa wakenya zaidi ya milioni 2.5 ambao wameorodheshwa vibaya na CRB.

  Kuanzishwa kwa adhabu ya kukomesha zoezi la kunyima wakopaji mikopo inakuja katika kipindi ambacho serikali inatarajia wakopeshaji kuongeza mtiririko wa pesa wa wafanyikazi na makampuni yaliyokuathirika na janga la Corona.

  Wakopeshaji wanaweza tu kunyimwa mkopo kwa sababu zingine zaidi na Watatarajiwa kuwajulisha wakopaji kwa kuandika juu ya sababu za kukataliwa kwa maombi yao ya mkopo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako