Jeshi la majini la Marekani limetoa onyo kwa meli zote katika Ghuba ya Uajemi kudumisha umbali usiopungua mita 100 na manowari za Marekani, la sivyo zitakabiliwa na hatari ya kuchukuliwa hatua halali za kujilinda.
Onyo hilo ambalo linaonekana kutolewa dhidi ya Iran, limekuja kufuatia rais Donald Trump wa Marekani kutishia mwezi uliopita kuangamiza boti za jeshi la Iran kama zikizisumbua manowari za Marekani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |