Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu UAE imetangaza kuwa chombo cha uchunguzi cha kuzunguka sayari ya Mars cha nchi hiyo kitarushwa Juli 15 kutoka kisiwa cha Tanegashima nchini Japan.
Chombo hicho ambacho ni cha kwanza cha aina yake cha UAE kilichotengenezwa kwa pamoja na UAE na Marekani, kinatarajiwa kuingia kwenye obiti ya sayari ya Mars mwanzoni mwa mwaka kesho, na kuanza utafiti wa kisayansi kuhusu hewa ya sayari hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |