• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa uongozi wa kikomunisti umesaidi sana taifa la China kupigana na umaskini

  (GMT+08:00) 2020-05-20 10:02:30

  Licha ya kuwa ni taifa lenya idadi ya juu zaidi ya watu duniani, ambayo ni takriban bilioni 1.3, China imejitahidi na kuhakikisha kwamba robo tatu ya wananchi wake hawako katika hali ya umaskini. Kila mwaka, China imekuwa ikiwaondoa mamilioni ya raia wake katika umaskini. Haya ni kwa mujibu wa bwana Muthiora Kariara, kinara wa chama cha The Great Nationhood Party, na pia mchambuzi wa masuala ya siasa na uchumi kutoka Kenya.

  Kulingana na bwana Kariara, kutokana na mfumo wa kikomunisti, serikali ya China ina nafasi nzuri ya kuweka mikakati ya kusaidia kujenga uchumi wake, ambao baadaye umesaidia sana kuinua hali ya maisha ya Wachina wote. Hii inatokana na uelewano uliopo katika uongozi wa mfumo wa kikomunisti.

  Vile vile, Kariara anasisitiza kuwa nafasi ya China katika vita dhidi ya janga la virusi vya corona kote duniani, imeonekana wazi kutokana na misaada waliotoa kwa zaidi ya mataifa 100 kote duniani. Hii ni hatua nzuri na ya kupigiwa mfano ikizaingatiwa kuwa, China imesaidia hadi mataifa ambayo yana uchumi na sekta za afya zilizo bora na imara.

  chache zilizopita ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba China inapaswa kubeba lawama na kulipia hasara za janga la corona, ni ya kupotosha mno. Haya ni kwa mujibu wa Bwana Cavince Adhere, Msomi wa Ushirikiano wa Kimataifa.

  Bwana Adhere anasema kwamba, kuishurutisha China kulipia hasara itokanayo na janga la corona, ni wazo ambalo halina msingi wowote. Kwani, uchunguzi unaonyesha kwamba chanzo cha virusi hivi bado hakijulikani.

  Kuhusu kuongezeka kwa maambukizi na vifo kutokana na virusi vya corona nchini Marekani, Bwana Adhere anasema kwamba Rais Trump hakuchukulia virusi hivi kwa uzito unaofaa. Aidha, licha ya mataifa mengine barani Uropa kuanzisha mikakati ya kujikinga na kuwapima raia wake, Marekani ilikawia kuchukua tahadhari na huenda hii ikawa sababu kuu ya kuenea kwa kasi kwa virusi vya corona katika taifa hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako