• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Rais wa TPBRC Joe Anea ajiuzulu

    (GMT+08:00) 2020-05-20 11:03:16

    Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), Joe Anea amejiuzulu nafasi hiyo. Anea ambaye alichaguliwa Machi mwaka jana kuongoza nafasi hiyo ameandika barua ya kujiuzulu kwenye kamisheni hiyo kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi. Katibu Mkuu wa TPBRC, Yahya Poli amethibisha kujiuzulu kwa Anea akisema aliandika barua ya kujiuzulu Jumamosi iliyopita na Jumatatu wakaijadili, na kwamba utaratibu wa kupata mrithi wake utaamuliwa kwenye kikao cha viongozi na wanachama wa TPBRC watajulishwa. Hata hivyo hivi karibuni kuliibuka tetesi kuwa Anea hana sifa za kuwa Rais wa TPBRC kwa vile anamiliki hati za kusafiria za nchi mbili tofauti, Tanzania na Uingereza, jambo ambalo ni kinyume na katiba ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako