• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kocha Mauricio Pochettino sasa yuko huru kujiunga na klabu yoyote anayotaka

  (GMT+08:00) 2020-05-20 11:04:06

  Kocha Mauricio Pochettino sasa yuko huru kujiunga na klabu anayotaka bila vikwazo kutoka kwa waajiri wake wa zamani Tottenham Hotspur baada ya marufuku ya miezi sita yaliyomzuia kufanya hivyo kukamilika.

  Pochettino, 48, amekuwa bila ajira tangu apigwe teke na Spurs mwezi Novemba 2019 kutokana na msururu wa matokeo duni. Raia huyu wa Argentina, ambaye aliIongoza Spurs kufika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya msimu 2018-2019, amehusishwa sana na klabu nyingine inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza, Newcastle United. Miamba wa Uhispania Real Madrid pamoja na mabingwa wa zamani wa Italia AC Milan wamekuwa pia wakiaminika kummezea mate Pochettino. Tottenham ilizuia klabu yoyote kumnyakua kabla ya miezi sita kukamilika kwa kuweka sharti kuwa klabu inayomtaka lazima iilipe timu hiyo kutoka kaskazini mwa London Sh1.6 bilioni ndipo iweze kumuajiri kwa sababu ilikuwa imemlipa Pochettino fidia ya kumtema kabla ya mkataba kutamatika. Kukamilika kwa miezi hiyo sasa kunamweka Pochettino huru kuchukuliwa na klabu yoyote bila ya ada kutolewa kwa Tottenham.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako