• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yailaani Marekani kwa kukiuka kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani

  (GMT+08:00) 2020-05-20 17:03:51

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo leo ametoa salamu za kumpongeza Tsai Ing-wen kuapishwa kuwa kiongozi wa Taiwan, akimwita rais wa Taiwan, na kupongeza "uhusiano wa kiwenzi" kati ya Marekani na Taiwan. Maofisa na wanasiasa wengine wa Marekani pia wametoa salamu za kumpongeza Tsai Ing-wen. Wizara ya mambo ya nje ya China imetoa taarifa, ikisema kitendo hicho cha Marekani kimekiuka kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, na taarifa tatu za pamoja zilizotolewa na China na Marekani, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

  Taarifa hiyo inasema, Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na China na Marekani wakati wa kuanzisha uhusiano wa kibalozi, Marekani ilikubali serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali halali pekee ya China, na Marekani inaweza kudumisha mawasiliano yasiyo ya kiserikali ikiwemo utamaduni na biashara na Taiwan.

  Suala la Taiwan linahusisha mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, na ni masilahi kuu ya taifa la China. Nia ya serikali na watu wa China ya kupinga ufarakanishaji wa Taiwan, na kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi haibadiliki, njia ya kupinga nguvu yoyote kuingilia kati mambo ya ndani ya China haibadiliki, na nia ya kutimiza umoja wa China bara na Taiwan haibadiliki. China imeionya Marekani kuwa, kuunga mkono Taiwan kujitenga na China hakika kutashindwa, na kitendo chochote cha kuharibu masilahi makuu ya China, na China itajibu kitendo chochote cha kuingilia kati mambo yake ya ndani kwa hatua yenye nguvu, na haiwezi kuzuia mkondo wa kihistoria ya umoja wa China. China inaitaka Marekani isahihishe makosa yake mara moja.

  Wizara ya ulinzi ya China leo pia imetoa taarifa ikilalamikia kitendo hicho cha Marekani, ikisisitiza kuwa, Jeshi la Ukombozi wa Watu la China lina nia imara, na imani na uwezo wa kutosha kushinda jaribio lolote la nguvu za nje kuingilia kati mambo ya ndani ya China na kuunga mkono ufarakanishaji wa Taiwan, na litachukua hatua yoyote ili kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi za China, na amani na utulivu wa sehemu ya Taiwan.

  Katika hatua nyingine, msemaji wa ofisi ya mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China Ma XiaoGuang leo amesema, hivi sasa uhusiano kati ya China bara na Taiwan ni tete, Chama cha Maendeleo ya Demokrasia cha Taiwan kinakataa kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, na Makubaliano yaliyofikiwa mwaka 1992 na China bara na Taiwan. Wakati huohuo, baadhi ya wanasiasa wa Taiwan wanachukulia janga la virusi vya Corona kama ni fursa ya kufanya ufarakanishaji. Vitendo hivi vinakiuka masilahi ya watu wa Taiwan na taifa la China, na kutishia amani na utulivu wa sehemu ya Taiwan. Ma amesisitiza kuwa, kutimiza umoja wa China ni kazi ya lazima katika mchakato wa kustawisha tena taifa la China, na hakuzuiliki na mtu yeyote na nguvu yoyote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako