Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kusaidia Afrika kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona.
Bw. Guterres amesema, mlipuko wa virusi hivyo kwa sasa barani Afrika bado uko katika kipindi cha mwanzo, na athari ya virusi hivyo itaongeza kwa kasi, hivyo ushirikiano wa jamii ya kimataifa na Afrika ni muhimu katika kukabiliana na hali ya sasa na kuhimiza kufufuka kwa haraka kwa uchumi katika bara hilo.
Pia amehimiza jumuiya ya kimataifa kuimarisha mfumo wa afya wa Afrika, kuhakikisha upatikanaji wa chakula, kuepuka mgogoro wa fedha, kuunga mkono elimu, kulinda ajira, kudumisha uendeshaji wa familia na makampuni na kulisaidia bara hilo kukabiliana na hasara ya kipato kinachotokana na biashara ya ndani na nje.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |