• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yawa nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu wenye maambukizi ya virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-05-20 17:52:11

  Russia imekuwa nchi ya pili duniani ambayo idadi ya wagonjwa waliothibitishwa imezidi laki 3.

  Taarifa iliyotolewa leo na Kituo cha Kushughulikia Maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Russia imesema, katika saa 24 zilizopita, wagonjwa 8,764 wapya walithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini Russia, na kufanya idadi ya jumla ya kesi za maambukizi kufikia 308,705.

  Taarifa hiyo imesema kuwa, idadi ya watu waliofariki imeongezeka katika saa 24 zilizopita na kufikia 2,972, na watu 85,392 wamepona. Aidha Russia imefanya upimaji wa virusi vya Corona kwa watu milioni 7.5 nchini kote.

  Habari nyingine zinasema, waziri mkuu wa Russia Bw. Mikhaïl Michoustine amepona na kuruhusiwa kuondoka hospitali, na ameanza kutekeleza majukumu yake kazini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako