• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Magufuli apongezwa kwa kufungua shughuli za kufungua utalii

  (GMT+08:00) 2020-05-20 19:42:36
  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamempongeza Rais wa Tanzania John Magufuli, kwa uamuzi wake wa kutaka baadhi ya shughuli muhimu za maendeleo ikiwamo sekta ya utalii kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya kukuza uchumi na pato la wananchi.

  Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Rashid Ali Juma, alisema kauli za Magufuli zimewatia moyo wananchi wengi na sekta muhimu ya utalii kwa kutaka kuona kwamba shughuli hizo zinarudi katika siku za hivi karibuni kwa sababu janga la ugonjwa wa corona limeanza kudhibitiwa.

  Naye Mwakilishi wa Jimbo la Konde, Omar Seif Abeid, alisema wakati umefika sasa kwa kamisheni ya utalii kujiweka sawa kwa maandalizi ya kuanza kufanya mawasiliano ya safari za watalii kuja nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako