• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za Afrika Mashariki zatakiwa kuongeza uzalishaji chakula

  (GMT+08:00) 2020-05-20 19:43:10
  Kenya Tanzania na Uganda zimeshauriwa kuongeza uzalishaji wa chakula ili kutosheleza mahitaji ya raia wake ambao idadi yao inaendelea kuongezeka.

  Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Climate Resilient Agribusiness for Tomorrow (CRAFT), nchini Tanzania Menno Keizer, kwamba kuna haja ya kujifunza kutumia uzalishaji unaoendana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuvuna mazao kisasa na kuchakata mazao ni masuala ya uzalishaji wa chakula na mifumo ya kukisambaza.

  Alifafanua kuwa ili kufanikisha ongezeko la uzalishaji wa chakula, kunahitajika ushirikiano wa wadau kufanya uwekezaji wa pamoja kuanzia wasambazaji, watoa huduma, wafanyabiashara kutoka sekta binafsi, na kuhakikisha kila mmoja katika nafasi yake anatekeleza wajibu wake ipasavyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako