• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: EU yatoa msaada wa kukabili nzige

  (GMT+08:00) 2020-05-20 19:43:40
  Kenya inatarajia kupokea shilingi bilioni 2.4 kutoka kwa Umoja wa Jumuiya kusaidia kupambana na nzige, na kusaidia wakulima walioathirika.

  Katika taarifa kwa vyombo vya habari, EU imesema kwamba nchi za Ulaya zimetenga shilingi bilioni 16 bilioni ili kusaidia uzalishaji wa chakula wa kutosha Kenya na nchi jirani.

  Msaada huo, ambao ulitoka, Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji, Ufaransa, Sweden na Denmark, utafikia wakulima na biashara ndogo na za kati.

  Tayari zaidi ya nchi 20 zimeathirika na misaada ya kifedha kama huo wa umoja wa Ulaya inatarajiwa kuleta utulivu kwa wakulima ambao wamepoteza mazao kutokana na uvamizi wa nzige.

  Mwezi uliopita, Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO, lilionya kwamba kundi jipya linalotarajiwa mwezi huu litakuwa kubwa zaidi ya mara 20 kuliko lile lililopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako