• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waafrika wanaokaa China wakati wa COVID-19 wapongezwa

    (GMT+08:00) 2020-05-20 20:23:20

    Mkuu wa Shirikisho la Urafiki kati ya Watu wa China na Nchi za Nje Bw. Lin Songtian amesema, katika kipindi muhimu zaidi cha Wachina kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, marafiki wengi za Afrika walichagua kubaki China na kujitolea kwenye mapambano hayo, na kushirikiana kwa pamoja na wenyeji na kuambia dunia ukweli.

    Tarehe 14, mwezi huu, Bw. Lin aliwaalika wanafunzi, madaktari, na wasanii wa kutoka nchi za Zimbabwe, Mauritius, Afrika Kusini na Sierra Leone waliopo nchini China kutembelea shirikisho hilo, kutembelea mtaa wa Wangfujing na kufanya mkutano wa kubadilishana maoni kuhusu mapambano hayo na mustakabali mzuri wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Baada ya kusikiliza jinsi waafrika hao walivyoshiriki kwenye mapambano dhidi ya virusi hivyo, Bw. Lin amesema, matendo mema ya vijana hao wa Afrika yameonesha mustakabali mzuri wa uhusiano wa China na Afrika. Vijana hao ni warithi, mashuhuda, na wanaofaidika na urafiki kati ya China na Afrika. Amesema, Afrika inaendelea kuinuka, na karne hii si karne ya Asia pekee, bali pia ni karne ya Afrika, ambayo imeingia kwenye kipindi cha maendeleo ya kasi ya viwanda na miji ambapo fursa nyingi zinatokea. Anatarajia waafrika hao kupata marafiki hapa China, kupata elimu, ufundi na kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya Afrika na urafiki kati ya Afrika na China.

    Bw. Lin amesema, hivi sasa, mlipoko wa virusi vya Corona unaendelea barani Afrika ambayo inahitaji ushirikiano wa kimataifa. Baadhi ya wanasiasa wa nchi za magharibi hawazingatia usalama wa afya wa Waafrika, wana wasiwasi kwamba, China itaongeza ushawishi barani Afrika kwa kutoa misaada ya kupambana na virusi hivyo, hivyo wanapaka matope ushirikiano na uhusiano kati ya China na Afrika. Bw. Lin amesema, China haitarajii wanasiasa hao wa Kizungu kuambia ukweli kuhusu China na kuisifu China, lakini inasikitika kuwa, marafiki wachache wa Afrika walipotoshwa nao, na kuishutumu China pamoja nao. Bw Lin anatarajia Waafrika walioko hapa China watasimulia hadithi zao, kujulisha hali halisi ya hapa China kwa jumuiya ya kimataifa, ili kuondoa kutoelewana na kutoa mchango kwenye ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya China na Afrika.

    Mwimbaji maarufu wa Sierra Leone Bibi Maria ameandika kwenye blog yake kuwa, alifurahia sana kupata mwaliko huo, na alijifunza mengi kutoka Bw. Lin. Amesema ndoto yake ni kufanya urafiki kati ya Afrika na China kuwa wa kindugu, na kueneza utamaduni wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako