• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: FUFA yamaliza ligi kwa kuitangaza Vipers mabingwa wa msimu huu

  (GMT+08:00) 2020-05-21 08:21:16

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) jana liliimaliza rasmi Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa kuitangaza rasmi timu ya Vipers kuwa bingwa wa msimu huu licha ya kila timu kubakisha mechi tano katika ratiba ya ligi. Uamuzi wa kuipa ubingwa Vipers umetangazwa na Rais wa FUFA, Injinia Moses Magogo katika mkutano wake na waandishi wa habari na wadau wa soka jijini Kampala. FUFA wamechukua uamuzi huo siku chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museven kutangaza kuongeza muda wa amri ya kukaa ndani kwa raia wake ikiwa ni mojawapo ya hatua za kukabiliana na virusi vya Corona. Kwa mujibu wa Magogo, kanuni iliyotumika kuipa ubingwa Vipers ni ile ya kuitangaza timu inayoongoza msimamo wa ligi kuwa bingwa ikiwa kila timu itakuwa imecheza angalau 75% ya mechi zote. Vipers itawakilisha katika Ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao wakati KCCA ambayo ipo nafasi ya pili, itacheza kombe la Shirikisho Afrika. Hadi Ligi ya Uganda inasimama, Vipers walikuwa wanaongoza msimamo wa ligi kwa pointi 54 wakati KCCA wakiwa na pointi 50. Kwa mujibu wa Magogo, timu tatu zinazoshika mkia katika msimamo wa ligi ambazo ni Maroons, Proline na Tooro United zitashuka daraja. Kamati ya Utendaji ya FUFA pia imetangaza kufuta ligi nyingine zote za soka nchini humo zikiwemo zile za vijana na wanawake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako