• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Bondia Fatuma Zarika ana usongo wa kuzichapa tena na bingwa wa taji la WBC duniani Yamileth

  (GMT+08:00) 2020-05-21 08:22:24

  Bondia Fatuma Zarika amesema kwamba bado ana kiu ya kuvaana na bingwa wa sasa wa taji la WBC duniani, Yamileth 'Yeimi' Mercado wa Mexico. Ni matarajio ya Zarika kwamba Yeimi ataridhia kurejea ulingoni kunyanyuana naye kwa mara nyingine licha ya promota wake kusitasita kukubali maombi hayo kwenye mchakato ulioanzishwa Januari 2020. Zarika alimzidi Yeimi maarifa kwa wingi wa alama walipochapana kwa mara ya kwanza Septemba 8, 2018 jijini Nairobi. Marudiano yaliyoandaliwa mjini Chihuahua, Mexico Novemba 16, 2019 yalimshuhudia Yeimi akilipiza kisasi dhidi ya Zarika aliyepokonywa ubingwa huo wa dunia. Hadi walipomenyana Novemba, Zarika alikuwa ameshikilia taji la WBC kwa kipindi cha miaka minne na kulitetea mara tatu tangu alitie kibindoni kwa mara ya kwanza mnamo 2016.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako