Mwenyekiti wa Baraza kuu la Shirika la Biashara Duniani WTO Bw. David Walker ameliambia baraza hilo kuwa mchakato wa uteuzi wa katibu mkuu mpya wa WTO utaanza rasmi Juni 8 na kufanyika kwa muda wa mwezi mmoja hadi Julai 8, ambapo watu wanaotaka kumrithi Bw. Roberto Azevedo watawasilisha maombi ya kugombea nafasi hiyo.
Baada ya mchakato huo kumalizika, Bw. Walker atawasilisha orodha ya wagombea wote kwa nchi wanachama, na wagombea wataalikwa kukutana na wanachama na kujibu hoja zao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |