Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana Jumatano alimwalika rais Mahmoud Abbas wa Palestina kuhudhuria mkutano wa kujadili suala la Palestina.
Shirika la habari la Palestina WAFA limeripoti kuwa pande nne, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Russia, zitakutana hivi karibuni bila kuweka ratiba halisi ya mkutano huo. Ripoti hiyo inasema Bw. Guterres alimwalika rais Abbas kushiriki kwenye mkutano huo kwa ajili ya kuandaa mkutano wa kimataifa wa ngazi ya mawaziri, ambao utajadili kwa kina suala la Palestina.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |