Rais Donald Trump wa Marekani jana Jumatano alisema anafikiria kuandaa mkutano wa kilele wa kundi la nchi saba G7 huko Camp David katika majira ya joto, ambao awali ulipangwa kufanyika kwa njia ya video kutokana na mlipuko wa COVID-19.
Rais Trump ametoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, wakati serikali yake inajaribu kufungua tena uchumi wa Marekani, licha ya idadi ya maambukizi ya COVID-19 nchini humo kuendelea kuongezeka na kuzidi milioni 1.5, na kusababisha vifo zaidi ya 92,000 hadi kufikia Jumatano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |