Rais Donald Trump wa Marekani amesema atakamilisha mpango wa kutumia dawa ya malaria aina ya hydroxychloroquine katika kujikinga dhidi ya COVID-19 ndani ya siku moja au mbili zijazo.
Rais Trump amekuwa akisema mara nyingi kuwa hydroxychloroquine inawezekana kutumiwa katika kuzuia COVID-19, licha ya onyo kuwa dawa hiyo inaweza kuleta madhara kwa moyo.
Mkurugenzi mtendaji wa mipango ya dharura ya huduma za Afya wa Shirika la Afya Duniani WHO Michael Ryan, ametoa onyo dhidi ya matumizi ya hydroxychloroquine au chloroquine, ambayo ni dawa za kutibu malaria na magonjwa mengine, kama tiba ya COVID-19, akisema dawa hizo zinatakiwa kutumiwa chini ya majaribio ya kikliniki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |