• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema itapanua vyanzo vyake vya fedha

    (GMT+08:00) 2020-05-21 09:19:43

    Baada ya Marekani kutishia kusitisha ada ya uanachama, mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Tedros Ghebreyesus, jana alisema katika miaka mitatu iliyopita WHO ilianza mageuzi ya kujaribu kupanua vyanzo vya kupata ufadhili, ili kukabiliana na changamoto ya kifedha.

    Bw. Tedros amesema bajeti ya WHO haizidi dola za kimarekani bilioni 2.3 kwa mwaka, ni sawa na bajeti ya mwaka ya hospitali yenye ukubwa wa kati ya nchi zilizoendelea, lakini shirika hilo linatakiwa kuhudumia dunia yote kwa kutumia bajeti yenye ukubwa huo.

    Bw. Tedros amesisitiza kuwa, tangu awe mkurugenzi wa WHO miaka mitatu iliyopita, siku zote amefanya juhudi kuhimiza mageuzi ya shirika hilo, ili kutafuta vyanzo vipya vya fedha, kupanua wigo wa ufadhili, hivyo shirika hilo lilitunga mradi wa kwanza wa uwekezaji, na litazindua mapema mfuko wa WHO ili kuchangisha fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako