• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia 30 ya watu wenye mapato ya chini mjini New York waambukizwa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-21 09:30:16

    Gavana wa Jimbo la New York Andrew Cuomo amesema hivi karibuni mji wa New York umefanya upimaji wa kingamwili dhidi ya virusi Corona, ambapo asilimia 27 ya watu wenye mapato ya chini wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

    Gavana Cuomo amesema matokeo ya awali ya vipimo hivyo kwa watu zaidi elfu 8 yameonyesha kuwa, katika eneo la Bronx ambapo wakazi wengi ni wamarekani wenye asili ya Afrika na Latin Amerika, asilimia 34 kati yao wamepimwa chanya, ikilinganishwa na kiasi cha wastani cha mji huo asilimia 19.9.

    Jamii ya Morrisania katika eneo la Bronx ina kiwango cha juu zaidi cha asilimia 43, na jamii ya Brownsville ya eneo la Brooklyn ina kiwango cha asilimia 41 cha maambukizi.

    Bw. Cuomo amesema matokeo hayo yanaonyesha kuwa hali ya maambukizi ya virusi vya Corona bado ni changamoto kubwa, na idara za afya zitashirikiana na jamii mbalimbali kufanya vipimo zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako