Katika mkutano na waandishi wa habari wa Shirika la afya duniani WHO, mkurugenzi wa kiufundi wa mradi wa dharura wa Afya wa WHO Bibi Maria Van Kerkhove amesema hivi sasa chanjo zaidi 120 za virusi vya Corona ziko kwenye hatua ya utafiti, idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi, na baadhi ya chanjo ziko katika tathmini ya kikliniki.
Bibi Maria amesema utafiti wa chanjo hauna njia ya mkato, ni lazima kufuata vigezo vya usalama na ufanisi, na hautakiwi kuruka hatua yoyote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |