Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetangaza kuwa limefikia makubaliano ya ushirikiano na kampuni ya Airtel Africa katika kuwasaidia watoto walioko Afrika kusini mwa Sahara kupata masomo kupitia mtandao wa internet.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, UNICEF na Airtel Africa zitatumia teknolojia na kuwanufaisha watoto milioni 133 walioko nchi 13 za Afrika kusini mwa Sahara kwenye kipindi cha janga la virusi vya Corona.
Taarifa iliyotolewa na UNICEF imesema hatua hiyo itahakikisha familia nyingi zaidi zinaweza kukabiliana na msukosuko wa afya na uchumi unaoletwa na janga hilo. Shirika hilo limesisitiza kuwa kufunga shule kutaathiri vibaya matokeo yaliyopatikana kwenye miaka kumi iliyopita katika kuongeza fursa za elimu kwa watoto.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |