• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya maambukizo ya virusi vya Corona yafikia 1029

  (GMT+08:00) 2020-05-21 10:10:00

  Kenya hivi sasa imeandikisha idadi ya maambukizo nchini humo hadi 1029 baada ya watu wengine 66 kupatikana na virusi hivyo hiyo jana. Akitoa tangazo hilo, waziri wa afya wa Kenya Bw Mutahi Kagwe amesema idadi kubwa ya maambukizo hayo imeshuhudiwa katika kaunti ya Mombasa ambapo kati ya watu 66 waliopatikana na virusi hivyo jana 30 ni kutoka Mombasa huku Nairobi ikiwa na maambukizo mapya 26.

  Waziri Kagwe amesema hii ni mara ya kwanza kwa Kenya kuandikisha idadi kubwa ya maambukizo kwa wakati moja na kuna haja ya hatua zaidi kuchukuliwa kukabiliana na kuenea kwa virusi hivyo.Maeneo mengine yanayoonekana kuwa changamoto kubwa katika vita dhidi ya virusi vya Corona ni Kajiado hasa katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga ambao unatumiwa zaidi na madereva wa malori wanaosafirisha bidhaa kutoka nchi moja hadi nyingine katika eneo zima la Afrika mashariki.

  "Idadi ya maambukizo leo kwa mara ya kwanza tanbgu tuanze kutoa taarifa imekuwa juu zaidi kwa kuwa tumeandikisha visa vingine vipya 66 ambapo 64 kati yao 64 ni wakenya na wageni 4. Mji wa Mombasa bado unaendelea kuongoza katika maambukizo ambapo kati ya maambukizo haya mapya 30 ni kutoka Mombasa na 26 ni kutoka Nairobi.Na kutokana na tatizo la madereva wa malori tumeandikisha visa vitatu katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga katika kaunti ya Kajiado".

  Kuongezeka kwa idadi ya maambukizo kunakuja wakati ambapo serikali imekuwa ikiendelea kuhimiza umma haja ya kuzingatia maagizo wanayotoa kila mara ili kujiepusha na virusi hivyo. Ili kudhiti hali kamati maalum ya kitaifa ya kupambana na virusi hivyo imetangaza kuendelea kwa marufuku ya kutotoka nje au kuingia katika eneo la Isili mjini Nairobi pamoja na mji wa kale mjini Mombasa hadi Juni 6 mwezi ujao. Waziri Kagwe anasema hii itasaidia kujua walioambukizwa na hatua za matibabu kuchukuliwa mara moja.

  "Ili kudhibiti zaidi maambukizo ya virusi vya Corona kamati ya kitaifa ya kukabiliana na corona imetangaza kuendelea kwa marufuku ya kuingia na kutoka nje katika eneo la Isili pamoja na mji wa kale wa Mombasa. Pia migahawa na misikiti yote itaendelea kufungwa hadi tarehe 6 mwezi ujao. Hii inalenga kusaidia kuleta udhibiti wa maambukizi katika maeneo hayo ambayo yameshuhudia idadi kubwa ya maambukizo".

  Wakati serikali ikiendeleza juhudi za kupambana na virusi vya Corona wakenya nao wanaonekana kufuata maagizo yanayotolewa huku wengi wao wakihakikisha kuwa wanavaa barakoa kila wakati. Hata hivyo katika mitaa duni bado kuna changamoto mbali mbali ambazo wakazi wanaonekana kukabiliwa nazo ikiwemo ukosefu wa maji na vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona kutokana na ukosefu wa fedha. Sauti ya wakazi wa mitaa duni

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako