• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mchezaji mkongwe zaidi kuwahi kufungia Uhispania astaafu soka

  (GMT+08:00) 2020-05-21 19:17:08

  Aritz Aduriz ambaye ni mwanasoka mkongwe zaidi kuwahi kufunga bao ndani ya jezi ya timu ya taifa ya Uhispania, amestaafu rasmi kwenye ulingo wa soka, wakati Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) ikiwa imesitishwa kwa muda kutokana na corona. Mchezaji huyo kwa sasa ni mshambuliaji wa klabu ya Athletic Bilbao inayoshiriki kivumbi cha Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga). Aduriz alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Bilbao ambacho kilipangiwa kuvaana na Real Sociedad kwenye fainali ya Copa del Rey mnamo Aprili 2020 kabla ya shughuli zote za soka kusitishwa kutokana na virusi vya homa kali ya corona. Aritz amejeruhiwa katika paja na kumfanya ashindwe kuendelea tena na soka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako