• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Golikipa na nahodha wa Bayern Munich atia saini mkataba mpya wa miaka mitatu

    (GMT+08:00) 2020-05-21 19:31:00

    Kipa Manuel Neuer wa Bayern Munich amerefusha mkataba wake na kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kwa miaka mitatu zaidi hadi Juni 2023. Kufikia sasa, Neuer, 34, anajivunia kunyanyulia Bayern mataji saba ya Bundesliga, matano ya German Cup na moja la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) tangu ajiunge na miamba hao wa soka ya Ujerumani kutoka Schalke mnamo 2011. Neuer ambaye ni nahodha wa Bayern, anasema anajihisi nyumbani zaidi akivalia jezi za waajiri wake wa sasa na anatazamia mambo mazuri zaidi kumtokea akiwa ugani Allianz Arena. Hadi kufikia sasa, Neuer anajivunia kuchezea timu ya taifa ya Ujerumani jumla ya mechi 92 na alikuwa tegemeo kubwa katika fainali kambini mwa kikosi hicho katika fainali za Kombe la Dunia zilizotawaliwa na Ujerumani mnamo 2014 nchini Brazil. Japo amekuwa chaguo la kwanza la Bayern kwa kipindi kirefu, Neuer atalazimika kukabiliana na ushindani mkali wa kuhifadhi nafasi yake katika kikosi cha kwanza msimu ujao baada ya kusajiliwa kwa chipukizi Alexander Nubel, 23, kutoka Schalke.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako