• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IATA yatoa miongozo ya kuanza tena kwa safari za ndege za kimataifa

  (GMT+08:00) 2020-05-21 19:32:58

  Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (IATA) limetoa mfululizo wa mapendekezo ambayo linasema yanaweza kusaidia sekta ya anga wakati ikijitayarisha kuanza ndege za abiria huku kukiwa na janga la maambukizi ya virusi vya Corona.

  IATA imechapisha Ripoti inayoitwa "Usalama kwa usafiri wa Anga :mpango wa kuanzisha tena usafiri wa anga",ambayo inaelezea pendekezo la shirika hilo la kuwekwa kwa hatua za muda mfupi za usalama.

  Mpango huo unalenga kutoa ujasiri ambao serikali za nchi mbalimbali utahitaji ili kuwezesha ufunguzi wa mipaka kwa usafiri wa abiria ,na ujasiri ambao wasafiri watahitaji ili kurudi kuanza kusafiri.

  Mpango huo unajumisha kila kitu kutoka kupima joto katika vituo vya kuingia,kudumisha upeanaji wa hatua ya umbali ya mita moja na nusu,ueuzi wa vifaa vya kugusa,na pia kutoa bidhaa za kujisafisha ndani ya ndege na katika viwanja vya ndege.

  Mkurugenzi Mkuu wa IATA , Alexandre de Juniac, alisema katima taarifa kuwa hakuna hatua moja itakayopunguza hatari na kuwezesha kuanza upya kwa usafiri wa ndege ulio salama,lakini hatua ambazo zinatekelezwa kote duniani na kutambulika na serikali zinaweza kuafikia matokeo yanayotakikana.

  Alisema COVID-19 ndio shida kubwa ambayo sekta ya anga imeshawahi kukumbana nayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako