• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Biashara zahesabu hasara kila siku wakati wa Ramadhan

    (GMT+08:00) 2020-05-21 19:33:16

    Huku zikiwa zimesalia siku chache kabla mwezi Mtzkufu wa Ramadhan kukamilika,ni wazi kuwa sherehe za Idd ul fitr zitakuwa tofauti mwaka huu.

    Maduka na masoko kwa kawaida huwa na shughuli si haba katika siku za mwisho kuelekea kuisha kwa mwezi wa Ramadhan.Maelfu ya watu hujazana kwenye maduka na masoko kununua nguo na chakula kwa matayarisho ya sikukuu ya Idd.

    Biashara mjini Mombasa ,ikiwa ni pamoja na katika soko maarufu la Mackinon au Marikiti,mjini na Kibokoni katika eneo la Old Town au Mji wa Kale ,huwa zinanoga wakati kama huu.

    Hata hivyo ,wafanyabiashara hivi sasa wanakabiliwa na hasara kubwa kufuatia hatua ya serikali ya kufunga maduka na masoko ili kudhibiti ueneaji wa maambukizi ya Corona.

    Maduka katika eneo la Eastleigh jijini Nairobi,Marikiti mjini Mombasa na soko la mifugo mjini Garissa yamefungwa.

    Wafnyabiashara hawa wametoa wito kwa serikali kuwaruhusu kufungua maduka yao na kuendelea na biashara huku wakizingatia hatua zote za kiafya zilizowekwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako